Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Corona kutibiwa kwa vidonge

COVID TAB.jfif Rasmi Corona kutibiwa kwa vidonge

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Mdhibiti wa Dawa nchini Uingereza, imethibitisha matumizi ya dawa za vidonge kwa ajili ya kutibu na kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Dawa hiyo iiyopewa jina la 'Molnupiravir', itakuwa ikitumika kutwa mara mbili kwa wagonjwa walioathirika na ugonjwa huo hasa wale wenye magonjwa mengine ambayo sio rafiki kama vile kisukari, uzito kuzidi na wale walio juu ya miaka 60.

Nayo Ofisi ya Wakala wa Udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya nchini Uingereza (MHRA) imesema kuwa dawa hiyo ni salama kutumika kwa wagonjwa walio katika hatari zaidi ya kupoteza maisha.

Tayari Serikali ya nchini humo imeshaanda dawa za kutosha zitakazotumika kutibu wagonjwa takribani 480,000.

Uingereza inakuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutumia dawa za vidonge kutibu ugonjwa huo na usambazaji kamili wa dawa hizo unatarajiwa kuanza kufanyika mwisho wa mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live