Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais THS aeleza umuhimu wa huduma ya afya kwa watu wote

Rais THS aeleza umuhimu wa huduma ya afya kwa watu wote

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Rais wa Kongamano la Afya Tanzania (THS), Dk Omary Chillo amesema ushirikiano unahitajika kati ya sekta ya umma na binafsi kubaini tofauti katika ubora, ufanisi na usawa kwenye  huduma za afya nchini.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 26, 2019 kuhusu kongamano la afya litakaloanza Mjini Dodoma kesho, Dk Chillo amesema tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini zinaonyesha umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti kufikisha huduma za afya kwa watu wenye kipato cha chini.

“Upo utafiti uliobaini kuwa asilimia 44 ya wenye kipato cha chini na cha kati hupendelea kusaka huduma za afya katika vituo binafsi vya afya hata kama gharama za matibabu ni ghali,” amesema.

Amesema ni lazima kujiuliza ni kwa nini watu hao hupendelea kwenda kwenye vituo binafsi kupata huduma za matibabu.

“Naamini kuna ushirikiano unahitajika baina ya sekta binafsi na umma ili kubaini tofauti zilizopo katika ubora, ufanisi na usawa ili tuwe na lengo moja tu la kumhudumia Mtanzania kwa ubora wa hali ya juu bila kujali kipato chake,” amesema.

Dk Chakou Halfani wa Taasisi ya Afya ya Tindwa (TMHS) atatoa mada kuhusu matumizi ya wasifu katika kuuza talanta au ujuzi miongoni mwa vijana katika kongamano hilo litakalowakutanisha wadau zaidi ya 500 wa sekta ya afya.

Chanzo: mwananchi.co.tz