Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia apeleka ambulance, CT SCAN na Digital X-Ray Hospitali ya Mount Meru

Gambo Mounttt At 17.jpeg Rais Samia apeleka ambulance, CT SCAN na Digital X-Ray Hospitali ya Mount Meru

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonyesha kujali afya za wananchi wake na hayuko tayari kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea kizembe.

Katika kutimiza ahadi zake zilizoko kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi hususan katika, Rais Samia ameipatia Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru gari la wagonjwa (ambulance) mpya, CT SCAN na Digital X-ray za kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu katika hospitali hiyo.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Jumatano, Novemba 29, 2023 na mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru, Dkt. Alex.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika hospitalini hapo, Gambo amesema; "Tunamshukuru sana Rais samia kwa kutupatia ambulance ya Kisasa kwa ajili ya Mount Meru Hospital. Tunamshukuru pia kwa CT SCAN na Digital X-ray kwenye Hospitali ya Mount Meru.

"Huduma za Afya ni muhimu ili kuunga mkono jitihada za Utalii kupitia Royal Tour! Pongezi kwa Wafanyakazi wa Mount Meru Hospital kwa kazi nzuri," amesema Gambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live