Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Wizara ya Afya ituambie tuendelee kuvaa barakoa au tupumzike

Samia Barakoa H Rais Samia Suluhu Hassan

Sun, 4 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais ameiagiza wizara hiyo kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na kutoa utaratibu kama bado kuna haja ya wananchi kuendelea kutumia barakoa.

Amesema; “Inaonyesha watu wamechoka nazo, niwaombe sasa Wizara ya Afya waangalie mwenendo huu tunaokwenda nao, lakini watathmini hali ilivyo halafu watuambie tuendelee kuwa nazo au kwa muda tupumzike.”

Hata hivyo, Rais Samia amewataka wale ambao hawajachanja wachanje kwa hiari ili kuweza kuwa kwenye hali nzuri ya kuzuia maambukizi ya janga hilo kwasababu bado ugonjwa upo na watu wajifunze kuishi nao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live