Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais John Magufuli kuzindia kituo cha afya Madaba

51318 Pic+kituo

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli anatarajiwa kuzindua kituo cha afya cha Madaba ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

Kituo hicho kilichogharimu Sh 665 milioni kina majengo ya wodi ya wazazi, maabara, upasuaji na kuhifadhia maiti.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege amesema kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya kutolea huduma za afya 352 vilivyokarabatiwa na kujengwa kupitia mpango  wa maboresho ya afya msingi.

“Tamisemi imeweka malengo ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa ngazi ya msingi kwa kukarabati vitoa vya afya 535 nchini ifikapo mwaka 2020,”amesema..

Balozi wa Canada nchini, Pamela O'donnel  ameipongeza Serikali  kwa kutambua kuwa afya na haki za wanawake na wasichana vijijini na kuwekeza kwao kwa ajili ya siku zijazo

“Ni heshima kubwa kwangu leo kuwa mmoja wapo katika kuzindua kituo hiki ifahamike kuwa huduma bora za afya zenye kufikiwa kwa kila mmoja ni muhimu kwa maendeleo, ”amesema.

Related Content



Chanzo: mwananchi.co.tz