Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mbeya aitaka MSD kudhibiti upotevu wa mapato

Msd Gh.jpeg RC Mbeya aitaka MSD kudhibiti upotevu wa mapato

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuvisimamia vituo vya kutolea huduma ili vikusanye mapato na kuchangiaji huduma za afya sambamba na mnyororo wa ugavi wa bidhaa.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Februari 09, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa kwa niaba ya Homera kwenye kikao kilichohusisha waganga wa wakuu wa mikoa na wilaya na wafamasia kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini.

Malisa amesema ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kila mmoja ana jukumu la kusimamia udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato na matumizi ya bidhaa za afya, ili kuleta tija kwa wananchi.

“Serikali imeendelea kuongeza fedha kwa ajili ya bajeti ya kununulia bidhaa za afya, dawa, vitenganishi na vifaatiba kuboresha utoaji wa huduma na kuleta tija kwa wananchi ili kuepuka na manung'uniko na upotevu wa mapato,” amesema Malisa.

Katika hatua nyingine, ameagiza waganga wakuu wa mikoa, wafamasia kukagua na kufautilia matumizi sahihi ya bidhaa za afya katika ngazi zote ili kudhibiti mianya ya upotevu wa bidhaa.

“Naagiza mkasimamie suala la ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze kulipa madeni yaliyopo MSD baada ya kupokea shehena za dawa, vifaatiba na vitenganishi na kuepuka madeni yasiyo ya lazima,” amesema Malisa.

Meneja wa MSD, Nyanda za Juu Kusini, Marco Masala amesema lengo la mkutano huo ni kupata fursa ya kujadiliana na kutatua changamoto za upatikanaji wa bidhaa za afya katika mikoa yetu.

“Mkutano huu utakuja na suluhisho la kuboresha upatikanaji wa bidhaa kwa lengo la kufikisha huduma bora kwa jamii ikiwa ni malengo ya Serikali ya awamu ya sita sambamba na kutoa tuzo kwa halmashauri ambazo zimetumia mapato ya ndani kununua bidhaa za huduma za afya,” amesema Masala.

Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe Joyce Wilson amesema wameweza kufanya vizuri katika uagizaji wa dawa MSD kwa kutumia mapato na ndani ya halmashauri na sio kutegemea fedha kutoka Serikali kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live