Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla apokea vifaa vya hospitali kutoka Ujerumani, avigawa Dar

Msaada Makalla RC Makalla apokea vifaa vya hospitali kutoka Ujerumani, avigawa Dar

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo amepokea Vifaa vya Afya ikiwemo Vitanda vya Wagonjwa, Meza za Wagonjwa na Vyuma vya kusaidia majeruhi wa Ajali kutoka Jiji la Hamburg Ujerumani ambapo Baada ya kupokea amevigawa kwa Halmashauri zote tano za Mkoa.

Akitoa mgawanyo wa Vifaa hivyo, RC Makalla amesema Jiji la Dar es salaam wamepata Vitanda 20, vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali na meza 7, Halmashauri ya Kigamboni Vitanda 28, meza 10 na vyuma 33 vya Wagonjwa wa Ajali na Halmashauri ya Kinondoni Vitanda 20, meza 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali.

Aidha RC Makalla amesema Halmashauri ya Temeke imepata Vitanda 20, Meza 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali huku Halmashauri ya Ubungo wakipata Vitanda 20, bedside 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali ambapo ameelekeza Vifaa hivyo kutumika vizuri.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo tayari Rais Samia Suluhu Hassan amefanya maboresho makubwa sekta ya Afya kupitia Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati na Vifaa hivyo vitakwenda kuongeza Nguvu sehemu hizo.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Kontena tatu Kati ya sita za Vifaa hivyo ambazo bado zipo bandarini zikombolewe kwa wakati ili lengo la kutolewa kwa msaada huo liweze kutimia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live