Geita. Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ameiomba Wizara ya Elimu nchini Tanzania kujenga chuo kikuu cha sayansi na tiba ya afya katika eneo inakojengwa Hospitali ya Rufaa Chato ili kuleta mapinduzi katika sekta ya afya.
Gabriel ametoa ombi hilo leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 katika ziara ya naibu Waziri wa Elimu, William Olenasha kukagua miradi ya elimu inayotekelezwa wilayani Geita.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kujengwa kwa chuo katika eneo hilo kutasaidia kuinua motisha katika mkoa huo ambao ulichelewa kuwa na vyuo kutokana na jamii kuwa na mwamko mdogo wa elimu
Akizungumzia ombi Olenasha amesema wazo la kuwa na chuo cha sayansi na tiba ni jambo jema kutokana na nchi kuwa na upungufu wa vyuo vya sekta ya afya.
Ameutaka uongozi wa Mkoa kuendelea na mchakato wa kutafuta ardhi kwa ajili ya ujenzi huku yeye alipeleka wazo hilo wizarani kuona namna ya kulifanya.
Akikagua ujenzi wa jengo udhibiti ubora wa elimu linalojengwa katika halmashauri ya Geita kwa gharama ya Sh150 milioni, Olenasha amesema wizara yake imetoa Sh760 milioni kwa ajili ya majengo 100 nchi nzima.
Pia Soma
- Wahofia kuondolewa kwenye maeneo ya kufanyia biashara
- Rais John Magufuli kuzindua Terminal 3 muda mfupi ujao
- Uhamiaji Tanzania yachukua paspoti saba nyumbani kwa Kabendera
- Serikali ya Tanzania yasaini mkataba ujenzi barabara ya lami Tanga - Pangani