Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Swai atoa mbinu kuepuka kisukari

10312 Rofessa+pic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha wagonjwa wa kisukari na umoja wa maradhi yasiyoambukiza, Andrew Swai amesema mbinu mojawapo ya kujikinga na kisukari ni kula matunda bila kuyasaga na kutokoboa nafaka.

Profesa Swai amesema hayo Juni 28, 2018 wakati wa mjadala kuhusu maradhi yasiyoambukiza wa Jukwaa la Fikra, ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

"Ukikoboa mahindi unapunguza wanga, vinakuwa havina faida na vinaweza kukufanya kukosa choo," amesema Profesa Swai.

Amesema, "Ukikosa choo kwa siku tatu ile sumu iliyotakiwa kutoka itabaki mwilini jambo ambalo ni moja ya visababishi vya saratani.”

Amesema kila mtu anatakiwa kuhakikisha kuwa sukari anayotumia kwa siku isizidi vijiko vitano.

Chanzo: mwananchi.co.tz