Profesa Mohammed Janabi, amekuwa akizungumza ukweli kuhusu namna ya kulinda afya, kuepuka magonjwa yasiyoambukiza, safari hii amekuja na soma jingine la kuepuka uzee.
Profesa Janabi, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasema hajawahi kukataza watu kula chakula.
“Sijawahi kusema watu wasile, bali nimesema watu wasile hovyo. Ni kweli nimesema watu wale kwa wastani, sasa ninarudia tena hivi vitu huwezi kuanza ghafla mara moja, ni kwenda taratibu na tunachoshauri zaidi sisi ni kupunguza vyakula vya wanga na kuepuka vyakula vya sukari,” anasema.
Anasema mtindo mbaya wa maisha na kula vyakula visivyofaa, inachangia kwa kiasi kikubwa watu kuzeeka mapema.
Profesa Janabi ameyasema hayo mapema wiki hii, alipofanya mahojiano maalumu na jarida hili. Anasema watu hawafi kwa sababu ya uzee, lakini wanakufa kwa sababu ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na mtindo wa maisha.
“Sijui kama kuna mtu amewahi kumuona mtu amekufa kwa sababu ni mzee, ilikuwa miaka ya zamani. Wengine Mungu aliwapa uhai mrefu, unamuona kabisa huyu ana afya yake.
Leo hii ninyi mnafahamu unaweza kukutana na mtu ana miaka 40 na mwingine miaka 30 ukadhani yule wa miaka 30 ndiyo ana miaka 45,” anasema Profesa Janabi na kuongeza:
“Mimi ukiniuliza kama daktari, ni kweli kwa miaka hii watu hawafi kwa sababu ni wazee, bali wanakufa kwa sababu ni wagonjwa. Ni mzee ana kisukari, ni mzee ana presha, ni mzee ana figo, wakati hata ukisikiliza dini zetu huko nyuma watu walikuwa wanaishi miaka 100, 200 na zaidi.”
Anasema hiyo inatokana na wengi kupenda vyakula rahisi na vya haraka na gharama nafuu, huku wakiumiza miili yao.
Anasema ni muhimu kutunza afya kuliko fedha, kwa sababu asilimia kubwa ya watu wanatunza fedha ili ziwasaidie uzeeni, huku akisisitiza kutunza afya zaidi ili iwafae uzeeni.
"Nafikiri ungetunza afya ikusaidie uzeeni kwa sababu hela hizi zitakuja kukusaidia kulipia gharama za kutibu magonjwa hospitalini, unafanya kazi miaka yote, unahangaika mjini miaka yote ili ukipata pesa uanze kuja kulipia betri za moyo! Nafikiri hiyo sio nzuri," anasema Profesa Janabi.
Mkurugenzi huyo anasema watu wengi wanamuelewa vibaya, hajawahi kuwakataza watu kula chakula, bali wale kwa wastani ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.
"Tunashauri kupunguza vyakula vya wanga, kuepuka vyakula vya sukari, vyakula vyetu vya kusindika ili viweze kukaa muda mrefu kwenye shelfu, lazima uweke kemikali, chumvi na sukari," anasema Profesa Janabi.
Anasema wengi wamekuwa wakichukulia mzaha na kwa bahati mbaya inapozungumziwa sukari, wanafikiria ni ile ya kununua na kuweka kwenye chai.
“Nimekuwa nikishauri sana Watanzania kuwa hebu wanaponunua kitu wageuze lile boksi upande wa nyuma wasome, kwa sababu vile vyakula vimeandikwa mchanganyiko wake, ikiwemo kiasi cha sukari, wanga, protini, hatuna hiyo tabia ya kusoma.
“Unaponunua chupa ya soda, geuza kule nyuma soma mchanganyiko wake ukoje, kwa sababu dhana moja, watu wengi hasa vijana wanasema haya ni magonjwa ya wazee, lakini hawako sahihi. Ili uweze kupata kisukari aina ya pili inahitaji miaka 15 mpaka 20 ya ulaji usiofaa,” anasema.
Profesa Janabi anasema kwa mtu anayejiita kijana akiwa na miaka 30, ina maana kisukari kitamkuta na miaka 50. “Ni magonjwa ya wazee ni kweli, lakini kwa hatua ya pili si kweli kwa sababau aliyekuwa na miaka 30 sasa ana miaka 50 anajikuta anaanza kutumia vidonge na sindano za kisukari.”
Anasema ujumbe wake ni vyema hivi sasa kila mtu awe na mpangilio, kama ni kunywa, alishauri kunywa bia moja kwa saa moja, lakini wengi wanafanya dhihaka, ilhali kunywa bia tano kwa saa moja kuna athari kubwa.
Anasema kila mmoja anayetumia kinywaji hicho anapaswa kutambua kuwa kinywaji hicho kinapanua moyo.
Anasema kilichomshangaza ni baadhi ya vyombo vya habari navyo kuirusha kwa kuitangaza na kuiandika habari hiyo kwa dhihaka.
“Mimi ni daktari wa moyo kwa zaidi ya miaka 20, ninawaona wagonjwa wanaoletwa hospitali moyo ukiwa umepanuka kwa sababu ya kileo, ninawaona wagonjwa tunawaondoa mapafu upande mmoja. Unakuta limekufa lote kwa sababu ya sigara,” anasema profesa huyo.
Hivyo, anasema kuna haja ya Watanzania kuchukua hatua ya kujikinga mapema ili kuwa na ahueni huko mbeleni.
“Tuchukue kinga tuwe na nguvu kazi mbeleni ya muda mrefu, ninataka Muhimbili baadaye tusitibu wagonjwa wengi. Badala ya kuniuliza mtambo gani mtauleta lini, bali ninachotaka ni watu waweze kuweka mfumo wa kutoa maji safi, wanywe maji safi,” anasisitiza.
Profesa Janabi anabainisha kwamba anatamani Muhimbili itoe kinga zaidi kwa Watanzania kwa kuelimisha jamii kwa kuwa wafanyakazi 3,600 wa hospitali hiyo wanaweza kutumika kutoa elimu sehemu mbalimbali nchini.
“Muhimbili tupo 3,600, tunaweza kutoa elimu kupitia kitengo cha umma, tukajipanga kuhusu kujikinga na magonjwa ya tezi dume, kiharusi, watu tubadilishe maisha yao, kuna vitu vichache tu, mtu atembee hatua 10,000 kwa siku.
“Kula kwa wastani, kupunguza wanga na kuepuka vitu vyenye sukari, kuepuka sigara, pombe, kupata muda wa kupumzika kidogo, ili uweze kufurahia maisha mbele ya safari. Ukiniuliza kama daktari, vitu hivi havihitaji hata senti tano,” anasisitiza.
Afya ya akili
Pamoja na mambo yote, Profesa Janabi anasema afya ya akili ni changamoto kwa sasa, huku akiitaja simu janja kuchangia kwa kiasi kikubwa.
Anasema suala la matumizi ya simu lina athari, kwa kuwa wapo watu wakiamka asubuhi kitu cha kwanza kukimbilia ni simu, akifika ofisini yuko kwenye simu, kabla hajalala usiku ana simu.
“Mawasiliano yamepungua sana kwenye nyumba zetu, unakuta kila mtu, baba, mama watoto kila mmoja yuko kwenye simu yake.
“Mawasiliano kama familia yamezidi kupungua. Kitaalamu, binadamu ana mawazo 70,000 kwa siku, bahati mbaya robo tatu ya hayo mawazo ni hasi. Ukiwa na mawazo hasi mengi inapunguza nguvu ya mwili,” anabainisha na kuongeza;
“Na kuelemea kwenye simu ni hivyo hivyo, unaweza kufungua ukakuta mtu kakutukana au kamtukana rafiki yako au vinginevyo.”
Akizingatia kukua kwa sayansi na teknolojia, Profesa Janabi anasema suala la kutumia simu, halizuiliki kwa wakati huu wa maendeleo ya teknolojia.
Hata hivyo, anashauri watu wachague vitu vya kuangalia, kuitumia kujifundisha vitu vya msingi. “Binafsi huwa najifunza vitu vingi sana kwenye simu, ikiwemo athari za magonjwa na mwenendo wake, dozi za dawa zinaendaje, siasa za ulimwengu zinaendaje, unaweza kuitumia vizuri kwa manufaa yako.”
Anasema matumizi ya simu yaliyozidi yanawafanya hata wazazi kushindwa kukemea watoto wasitumie simu kwa sababu na wao muda mwingi huutumia kwenye peruzi simu.
“Tuanze kubadilika, unafika nyumbani kwa saa kadhaa hakuna mtu kugusa simu ili kuruhusu wanafamilia kuwasiliana. Mbona sisi wakati tunakua hakukuwa na simu lakini maisha yalikuwa mazuri tu?” anahoji Profesa Janabi.
Profesa Mohammed Janabi, ambaye amekuwa akizungumza ukweli kuhusu namna ya kulinda afya, kuepuka magonjwa yasiyoambukiza, safari hii amekuja na soma jingine la kuepuka uzee.
Profesa Janabi, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasema hajawahi kukataza watu kula chakula.
“Sijawahi kusema watu wasile, bali nimesema watu wasile hovyo. Ni kweli nimesema watu wale kwa wastani, sasa ninarudia tena hivi vitu huwezi kuanza ghafla mara moja, ni kwenda taratibu na tunachoshauri zaidi sisi ni kupunguza vyakula vya wanga na kuepuka vyakula vya sukari,” anasema.
Anasema mtindo mbaya wa maisha na kula vyakula visivyofaa, inachangia kwa kiasi kikubwa watu kuzeeka mapema.
Profesa Mohammed Janabi akizungumza katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na Mwandishi Herieth Makwetta, alipofika ofisini kwake katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga.
Profesa Janabi ameyasema hayo mapema wiki hii, alipofanya mahojiano maalumu na jarida hili.
Anasema watu hawafi kwa sababu ya uzee, lakini wanakufa kwa sababu ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na mtindo wa maisha.