Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Janabi: Kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa si afya

Prof. Janabi Muhi Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema Wajawazito wanaojifungua Watoto Wanene wasidhani Watoto wao wana Afya njema

Amesema "Pale Wodini unakuta mtu amejifungua Mtoto ana Kilo 4, ndugu wanasema Mashallah, hapo hakuna Mashallah, Mtoto ni 'Over Weight' huyo, si jambo la kufurahia ni tatizo hilo. Si sahihi kwa Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa kupita kiasi"

Ameongeza kuwa unene uliopitiliza kwa Mtoto unamuweka hatarini kuja kupata Magonjwa Yasiyoambukiza yakiwemo ya Figo, Moyo, Shinikizo la Juu la Damu pamoja na Kisukari anachoweza kupata kutoka kwa Mama

Aidha, ameshauri Wajawazito kuzingatia ulaji mzuri wa Vyakula kwasababu una athari za moja kwa moja kwa Mtoto atakayezaliwa.

Chanzo: Mwanaspoti