Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof. Lipumba apata chanjo ya corona

Lipumba Pc Data 660x400.jpeg Prof. Lipumba apata chanjo ya corona

Thu, 22 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo Jumatano Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(UNICEF), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

“Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao, hivyo na mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezeaha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, “ Profesa Lipumba.

MTOTO MDOGO WA GIFT ALIYEUAWA ASIMULIA ALICHOAMBIWA NA BABA YAKE KABLA HAJAFA, MAMA ATOA YA MOYONI

Chanzo: millardayo.com