Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polyclinic zapewa onyo udanganyifu bima ya afya

3c55ab6dd5178655f351aeb9953b7e0d.jpeg Polyclinic zapewa onyo udanganyifu bima ya afya

Sat, 9 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa kliniki zinazotoa huduma za kawaida na za kibingwa (polyclinic) zilizosajiliwa na kuhudumiwa na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) kuepuka udanganyifu ili kuepusha mfuko huo kufi lisika.

Aidha, alisema serikali ipo katika mpango wa kuanzisha Baraza la Usuluhishi na Utatuzi wa migogoro litakalosaidia kutatua malalamiko yanayotolewa na pande zote wakiwemo watoa huduma, NIHF pamoja na wananchi.

Ummy alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano baina ya NHIF na watoa huduma ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haina nia ya kuzifungia polyclinics isipokuwa zinapaswa kufuata utaratibu uliowekwa katika utoaji wa huduma.

“Kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na polyclinic nchini. Wapo baadhi wenye nia njema nabaadhi wadanganyifu ambao dhamira yao ni kuona NHIF inafilisika suala ambalo katu hatutolikubali, ipo mifano mingi kuzihusu,” alisema Ummy.

Alisema ili kuhakikisha polyclinic hizo hususani zilizosajiliwa zinaendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma, utawekwa utaratibu mzuri kwa lengo la kuzibana ili ile dhamira ya kuanzishwa kwake iweze kutekelezeka kwa ufasaha bila kuathiri pande zingine.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema mkutano huo baina ya NHIF na wadau hao ni wa kawaida ukilenga kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu utoaji wa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live