Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania, chuo cha Aga Khan wazindua kampeni kupima afya bure

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) limezindua kampeni ya kupima afya bure kwa maofisa wa jeshi hilo, watumishi na wananchi.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, maofisa na wakaguzi wa polisi imezinduliwa leo Jumatano Julai 31, 2019 na kamishna wa polisi, utawala na menejimenti ya rasilimali watu, Benedict Wakulyamba.

Wakulyamba aliyemwakilisha Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amesema lengo la kampeni hiyo ya siku tatu ni kuwawezesha askari kutambua afya zao.

“Njooni mtambueni afya zenu, watu wengi wamekuwa waoga kuja kupima wakidhani  wakijua matatizo yao watadhalilika. Sisi tunataka mwatumikie wananchi mkiwa na uhakika wa afya zenu,” amesema kamishna huyo.

Mtaalamu wa afya na akili na mhadhiri wa AKU, Profesa Tumbwene Mwansisya amesema kampeni hiyo itatoa fursa kwa wananchi kufahamu afya zao na kutambua matatizo yao mapema.

Chanzo: mwananchi.co.tz