Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha:Waziri wa Afya azindua kiwanda cha kuzalisha Barakoa

Pic 3 660x400 Picha:Waziri wa Afya azindua kiwanda cha kuzalisha Barakoa

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Dorothy Gwajima amezindua Kiwanda cha Vifaa Tiba Mony Industries chenye uwezo wa kuzalisha Barakoa 100 kwa dakika Moja.

Katika uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Uvumba Street-Kigamboni, Waziri Gwajima amesema Alisema..“ Nipende kuwajulisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia ipo katika kuunga mkono juhudi hizi kwani imeweka kipaumbele katika sekta ya afya,

“Vile vile nitoe wito kwa wanachi wa Tanzania kuzingatia umuhimu wa afya zao binafsi kwani takwimu zinaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote vinavyotokea nchini,”- Waziri wa Afya

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mony Industries, Violet Mordichai alielezea kwa kina ubora wa bidhaa zinazotokana na kiwanda hicho zinazofanya kiwanda hicho kuwa na uwezo wa kuhimili ushindani wa ndani na nje ya nchi.

“Tuna mashine 7 za kisasa zenye uwezo wa kuzalisha barakoa 100 kwa dakika 1 huku kikiwa na uwezo wa kuzalisha Barakoa za Hospitalini (Surgical Masks), Viwandani (KN 95) na za Umma kwa Ujumla (Medical Masks). Na hivi karibuni kitaanza kutengeneze glavu za (Surgical na Medical), kwa hivyo kuweza kuhimili soko la ndani na la kimataifa ikiwa ni mpango wa hivi karibuni”- Mkurugenzi

.

.



.



.

.



.

KAULI YA KAGAME KABLA YA WANAJESHI WAKE 4 KUUAWA MSUMBIJI “SISI KUPOTEZA MTU MMOJA NI KITU KIKUBWA”
Chanzo: millardayo.com