Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pera linavyoimarisha kinga ya mwili

Pera Linavyoimarisha Kinga Ya Mwili.png Pera linavyoimarisha kinga ya mwili

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Mwananchi

Tunafahamu matunda yenye vitamini C husaidia kuimarisha kinga ya mwili na kuharakisha uponaji kwa haraka.

Lakini ulishawahi kujiuliza siku ukikosa machungwa ambayo wataalamu wa masuala ya afya wanatueleza kuwa yamesheheni vitamini C, unaweza kutumia matunda gani yatakayokusaidia kupata vitamini C kwa wingi?

Jibu hili hapa, matunda kama mapera, maembe, mananasi, ukwaju, mabungo, ubuyu na zabibu, machenza, limao na ndimu yatakupa vitamini C ya kutosha.

Ofisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Medina Wandella anasema mojawapo ya faida ya kula matunda yenye vitamini C ni kuimarisha kinga ya mwili na kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali, likiwamo Uviko-19.

Chanzo: Mwananchi