Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panya buku 22 wagunduzi wa TB wapelekwa Msumbiji, Ethiopia

11879 BUKU+PIC TanzaniaWeb

Sat, 21 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kimepeleka panya buku 22 wenye uwezo wa kutambua bakteria wanaosababisha Kifua Kikuu, (TB) katika nchi za Msumbiji na Ethiopia.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Julai 21, 2018  katika kongamano la kwanza la watafiti waliojikita kuchunguza TB na Ukoma lililoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mtafiti kutoka Kituo cha Udhibiti wa viumbe hai waharibifu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA-APOPO), Dk Georges Mgode, amesema panya buku hao wameshafanya kazi kadhaa za kugundua sampuli za makohozi yenye bakteria wa TB ambao hawakugundulika kupitia vipimo vya kawaida.

“Tunao panya hawa hapa Tanzania, teknolojia hii pia inatumika huko Msumbiji ambako jumla ya panya 12 wanasaidia kufanya utafiti na Ethiopia tumepeleka panya 10 mwaka huu, pale SUA tuna panya 40 na wengine tisa wapo katika maabara yetu iliyopo hapa Dar es Salaam.”amesema.

“Pale SUA tunafanya kazi ya upimaji na tafiti kwa ugonjwa huu kwa kutumia panya hao ambao tumewapatia mafunzo maalum.”

Amesema,  “Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa TB duniani na ndiyo maana tunawakutanisha watafiti ili wajadili na kutoka na mapendekezo yatakayoisaidia wizara tutoke tulipo.”

Amebainisha kuwa kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wa mwaka 2016,  kuna wagonjwa 160,000 wapya wa TB kwa mwaka lakini uwezo wa kuwatambua ni wagonjwa 65,500 sawa na asilimia 41 tu.

“Kuna wagonjwa 96,000 ambao hatuwagundui, changamoto ni kwamba wengi hawaendi hospitalini na wapo ambao huenda kwa waganga wa kienyeji lakini wale wanaokuja asilimia 90 hupona kabisa,” amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz