Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamoja na maboresho bado kuna changamoto kuvifikia vituo vya afya

E412b9aac20db6345521b65b31f4986e Pamoja na maboresho bado kuna changamoto kuvifikia vituo vya afya

Wed, 25 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na serikali katika kuboresha huduma ya afya kwa wananchi bado kuna baadhi ya watu wanashindwa kuvifikia vituo vya afya ili kupata huduma za kitabibu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Mabula Nchembe amesema hayo hii leo wakati akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) jijiji Dodoma, lenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya afya hasa kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati.

Prof Nchembe amewataka washiriki wa kongamano hilo kuhakikisha wanajadili namna ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo kuboresha vifaa na miundombinu katika hospitali zote nchini.

"Kupitia kongamano hili naomba mjadilii na kutoa mapendekezo ya namna ya kuwasaidia watu wa hali ya chini hasa wakulima ambao hawana bima ya afya pamoja na kutozifikia huduma za afya kiurahisi" amesema Prof Nchembe.

Chanzo: habarileo.co.tz