Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha waliozaliwa ndani ya beseni wafariki dunia

14633 Pacha+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Watoto pacha waliozaliwa kwenye beseni wilayani Misungwi mkoani hapa wamefariki dunia wakati wakipata matibabu Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Mama wa watoto hao, Winfrida Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Mwagala wilayani hapo alijifungua watoto hao kwenye beseni akiwa wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi baada ya kukosa huduma. Watoto hao walizaliwa Agosti 27 asubuhi.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 30 mama mzazi wa Winfrida, Flora Lugwisha amesema watoto hao wamefariki usiku wa kuamkia leo.

Amesema aliyetangulia kufariki ni Dotto ambaye utumbo wake ulikuwa nje na badaye alifariki Kulwa.

“Tupo hapa Bugando, lakini wamefariki dunia, maana walikuwa wananyonya kwa kutumia mpira,” amesema Flora.

Amesema madaktari waliwaeleza kwamba hawawezi kumshona kwa sababu tumbo bado ni dogo.

Hata hivyo, ofisa uhusiano wa Bugando Lucy Mogele kwa nyakati tofauti amekuwa akisema hawana taarifa za watoto hao kulazwa hospitalini hapo.

Soma Zaidi:

Ajifungua watoto pacha kwenye beseni, mmoja utumbo upo nje

 

Chanzo: mwananchi.co.tz