Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha walioungana watenganishwa Saudi Arabia

33375 Pic+pacha Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Pacha walioungana, Anishia na Melanese wametenganishwa nchini Saudi Arabia Desemba 23,2018 na hali zao zinaendelea vizuri.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Desemba 25, 2018 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amethibitisha pacha hao kutenganishwa.

Kwa mujibu wa gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette.com pacha hao walitenganishwa na jopo la wataalamu 32 kwa muda wa saa 13.

Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya Mfalme Abdullah, (King Abdullah Children’s Specialist Hospital) iliyopo katika mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.

Pacha hao wa kike waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Missenyi, Kagera, Januari 2018 walipofikishwa Saudi Arabia walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya kuona uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.



Chanzo: mwananchi.co.tz