Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PIRAMIDI YA AFYA: Ugonjwa wa baridi yabisi na karaha kwa wazee

58071 Shita+Samweli

Fri, 17 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kwa waliobahatika kutembelea nyumba za wazee wasiojiweza ni kawaida kukutana na mzee ambaye ukimtazama, utaona ana maungio yasiyo ya kawaida ikiwamo kupinda vidole na kuota vichuguu katika maungio ya mikono.

Kuna uwezekano mzee mwenye maumbile hayo ana ugonjwa wa baridi yabisi, tatizo linalotokea baada ya kinga ya mwili ya kawaida inaposhambulia tishu za mwili ikiwamo maungio, nyuzi ngumu za miishilio ya misuli na mifupa.

Matokeo ya hali hii ni shambulizi sugu na uharibifu wa tando za tishu za maungio (joint) pamoja na tishu zingine zinazozunguka na kuunda maungio ya mwilini. Ugonjwa huu huathiri maungio ya pande mbili kwa mpigo yaani kama na maungio ya mikono huwa pande zote, kulia na kushoto.

Ugonjwa huu unajulikana kitabibu kama Rheumatoid Athritis, huzifanya tishu hizo kuganda na kutengeneza vichuguu, jambo ambalo baadaye huwa na madhara mabaya.

Hii nikutokana na kuathiri maungio ya mwili na kushindwa kufanya kazi yake na pia huweza kumpa mtu ulemavu wa kudumu endapo hatapata tiba mapema.

Tatizo hili huwapata zaidi wanawake watu wazima pamoja na watu wengine vijana wa jinsia zote. Chanzo hasa cha kutokea tatizo hili huwa hakijulikani, ingawa vipo vihatarishi vya kupata tatizo hili kuanzia kati ya miaka 30-50 na wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

Pia Soma

Ugonjwa huu huanza taratibu na hujitokeza baada ya majuma kadhaa mpaka miezi. Athari zake hutokea katika pande mbili za viungio husika.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na maumivu, kuvimba na kukamaa katika maungio madogo ya mwili ikiwamo ya vidole vya mikono na ungio la kiganja cha mkono. Dalili hizi huwa zaidi nyakati za asubuhi. Kukamaa kwa maungio huweza kujionyesha kupata nafuu pale unapolazimisha kufanya kazi kwa nguvu zaidi.

Vifundo vinaweza kuonekana kubadilika na kuwa vyekundu na kuwa na joto kuliko maeneo mengine ya mwili. Kujihisi kuchoka kwa kipindi kirefu.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

Chanzo: mwananchi.co.tz