Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PIRAMIDI YA AFYA: Kwa nini wanawake hupata tatizo la kutofika kileleni?

81652 Shita+Samweli PIRAMIDI YA AFYA: Kwa nini wanawake hupata tatizo la kutofika kileleni?

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kufika kileleni au kufika mshindo kwa lugha ya kitabibu hujulikana kama orgasm na kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama ‘coming’ au ‘climaxing.’

Ni tukio ambalo linahusisha upitaji wa hatua kadhaa wa usisimuliwaji wa kimwili na kiakili.

Ni kawaida katika jamii kuwapo kwa malalamiko ya ndani kwa ndani kuhusiana na tukio zima la wenza wawili kutofika kileleni na kiridhika.

Tafiti zinaonyesha wanawake ndiyo wanapata zaidi tatizo hili kuliko wanaume na huona aibu kulishitakia katika huduma za afya.

Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 10-15 ya wanawake duniani hawajawahi kufika kileleni.

Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee unaoleta hisia nzuri kwa wenza wawili wanaowajibika kikamilifu katika tendo la ndoa. Hisia hizi hutokea kwa wenza wote kama ishara ya kufikia kilele cha tendo na kuridhika.

Pia Soma

Advertisement
Hisia hizo huambatana na mtiririko wa matukio kadhaa yanayohusisha mfumo wa fahamu (ubongo na mishipa ya neva), damu na moyo, vichochezi na maeneo mengineyo ikiwamo viungo vya uzazi.

Wenza wanapofika kileleni mapigo ya moyo hubadilika, hudunda kwa haraka na huku upumuaji ukiwa ni wa kasi na kuvuta pumzi kwa nguvu.

Kwa wanawake hali hii huwa ni nzito na yakipekee, kufika kwao kileleni nakupata hisia nzuri huweza kuambatana na kujikunja ama kujikaza kwa misuli ya maeneo ya ukeni, nyumba ya uzazi na kiunoni.

Mwanamke anaweza kufika kileleni zaidi ya mara moja muda mfupi tu tangu alipofika kileleni mara ya kwanza na ataendelea kupata hisia hizo endapo ataendelea kusisimuliwa, hisia hizi hudumu kwa sekunde 15-60.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

Chanzo: mwananchi.co.tz