Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

P2 yaongoza kutumiwa na wanafunzi

P2 B P2 yaongoza kutumiwa na wanafunzi

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imesema inafanya utafiti wa Dawa za nguvu za kiume aina ya Viagra kwa kuangalia matumizi yake kwa ukubwa na yapo kwa kiasi gani, ili waweze kutoa elimu sahihi kwa jamii.

Pia wameziwekea mkakati dawa aina ya P2, kwa lengo la kudhibiti uholela wa utumiaji wake ambapo, imeonekana watoto wa shule wengi wanapenda kuzitumia kutolea mimba.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Adam Fimbo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46, ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Alisema utumiaji holela wa dawa za jamii ya kutolea mimba na za kuongeza nguvu za kiume, zimekuwa zikitumika ndivyo sivyo na kuwaleta madhara watu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live