Taasisi ya udhibiti wa dawa barani Afrika,Africa Medicines Agency limeonya kukithiri uwepo wa dawa bandia barani hali inayokwamisha mapambano ya usugu wa vimelea vinavyosababisha magonjwa tofauti hivyo kuongeza gharama ya huduma za afya na hatari ya vifo vinavyotokea barani
Mkuu wa taasisi ya afya katika AU, Chimwemwe Chamdimba, akizungumza katika kongamano la afya jijini Lusaka ,amesema utafiti uliofanywa na AU kwa ushirikiano ya IGAD umebainisha dawa za kuwasaidia akina mama wanapojifungua Oyctocin asilimia 26 ni bandia huku dawa ya antibiotic maarufu Amocillin zaidi ya asililimia 76 haziijaidhinishwa na taasisi za udhibiti dawa.
“Uwepo wa dawa muhimu kwa jamii lazima ulingane uhitaji wake,kwa sababu iwapo sipati dawa halali,nitalazimika kupata dawa yoyote nitakayopata ,ni swala ni kitu ambacho hakiwezi kushughulikiwa kitaifa ,tunajenga mtandao wetu kiukanda kupambana na dawa bandia,kubadilishana taarifa na kukabiliana na ulanguzi wa dawa bandia nje ya mipaka tofauti,hali tuliyoshuhudia Gambia ambapo wanetu walifariki kutokana na dawa ya homa haiwezi kukubalika Afika,” alielezea Chimwemwe .
Taasisi hiyo mpya ya udhibiti wa dawa barani Afrika ,Africa Medicines Agency, itakayosimamia udhibiti na ukadiriaji ubora,inatazamiwa kumwajiri hivi karibuni mkurugenzi mkuu na tayari ina kamati kumi za kiufundi zinazoendelea na kazi.
Miongoni mwa kamati hizo ni kamati kuhusu ufuatiliaji wa usambazaji wa dawa kwenye soko na usajili wa dawa hizo.
Taasisi hizo zimeonya hali hii inaathiri ufanisi wa matibabu wa magonjwa na kuwaweka wengi kwenye hatari ya kupoteza maisha.
Profesa Sam Kariuki mtaalam kuhusu maswala ya usugu wa vimelea pia mkurugenzi katika shirika la DNDI linaloshughulika na dawa za magonjwa yaliyotengwa, amesema usugu wa vimelea unakuwa gharama isiyohitajika kwa serikali za Afrika,hela ambazo zingetumika kufanya miradi ya kimaendeleo.
“ Dawa zetu zote zinaagizwa kutoka mataifa mengine na tunatumia pesa nyingi kuagiza,tunapopata dawa zinakuwa hazifanyi kazi ,mara moja tunaweza wapoteza watu ,utafiti tuliofanya ulionesha thuluthi tunaweza kupoteza thuluthi moja ya watu ambao hawakutibiwa.” alisikitika profesa Kariuki aliyewahi kuwa mkuu wa taasisi ya utafiti wa matibu nchini Kenya,KEMRI.
Watafiti wa matibabu mbali mbali wanawasi wasi pia kuhusu hili.
Dkt Kenson Kipchumba anafanyia kazi shirika linalofanya utafiti na majaribio ya matibabu ya Victoria Biomedical Research jijini Kisumu ,Kenya,amesema tatizo hili ni pigo kwa watafiti wanaopambana kutafuta matibabu mapya.
Ametoa mfano wa utafiti waliofanya nchini Kenya unaonesha kuwa wagonjwa waliokuwa wanatibiwa magonjwa yanayoathiri, mishipa ya mkojo wengi wao wamekuwa wakirudi kutibiwa zaidi ya mara moja .
“Tunataka sana kuleta sokoni dawa kwa raia kwa bei nafuu lakini unapopata dawa ambazo zinatumika kutoa tiba zinafikia kiasi haziwezi kutumika ni changamoto kubwa,” alisema Daktari Kipchumba.
Wanayasansi hao pia wanaonya kuwa dawa za kutoa tiba daraja la pili ni ghali mno na hazipatikani kwa urahisi.
Oktoba mwaka huu,shirika la afya duniani WHO lilipiga maarufuku matumizi ya dawa ya kikohozi ya watoto ya maji, kutoka India baada ya vifo vya watoto wanne nchini Gambia.