Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

 ‘One Stop Jawabu’ yaibua wenye shinikizo la damu

Ce2f7aaedd915cb43c83949e5eea0e34 ‘One Stop Jawabu’ yaibua wenye shinikizo la damu

Wed, 23 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imewaibua watu 21 wenye matatizo mbalimbali ya moyo, 18 wamekutwa na shinikizo la damu, walipochunguzwa afya zao katika Viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke katika jukwaa la ‘One Stop Jawabu.’

Akizungumza na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu alisema watu 16 kati ya 18 waliokutwa na shinikizo la damu walikuwa hawajitambui kwamba wanakabiliwa na tatizo hilo.

"Hii ni sawa na asilimia 18, yupo mmoja ambaye tumemkuta ana shinikizo la damu 200 chini ya 110, ni mara yake ya kwanza amekuja kufanyiwa uchunguzi, ni shinikizo ambalo lipo juu mno, tulidhani labda amepata mshituko alipofika hapa,” alisema.

Akaongeza:"Tulimtaka akae kidogo apumzike, tukamfanyia tena uchunguzi na kukuta hali ikiwa vile vile, endapo tusingemgundua alikuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha, tumempa rufaa kuja JKCI kwa matibabu."

Dk Rweyemamu alisema mtu mmoja kati ya hao walifanyiwa uchunguzi amekutwa na tatizo la kuziba kwa mshipa wa damu kwenye moyo, watu 10 wamekutwa na kisukari.

"Watu 50 tuliwachunguza afya ya moyo kwa kutumia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO) na 53 tuliwafanyia kipimo cha kuangalia umeme wa moyo (ECG) wawili kati ya hao tuliowachunguza tulikuta 'valve' zao za moyo zina tatizo," alibainisha.

Akaongeza: "Asilimia 50 ya watu wote tuliowachunguza wana uzito uliopitiliza, hii ni hatari kwa afya ya mioyo yao. Watu 21 tumewapa rufaa kuja kwenye taasisi yetu kupitia hospitali yao ya Mbagala Zakheem ili tuwafanyie uchunguzi zaidi na kuwapa matibabu.”

Chanzo: habarileo.co.tz