Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ocean Road yaokoa bil 6/- tiba za kibingwa

Ba991e029972565ab50f436f8cb2856d Ocean Road yaokoa bil 6/- tiba za kibingwa

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam imeokoa Sh bilioni sita kutokana na maboresho ya huduma za kibingwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk Julius Mwaisalage alisema kutokana na maboresho hayo idadi ya wagonjwa kutoka nje ya nchi wanaokwenda kufuata tiba za kibingwa wameongezeka.

Dk Mwaisalage alilieleza gazeti hili kuwa, awali walikuwa wanapokea wagonjwa 70 hadi 80 kwa mwaka, lakini sasa wamepokea wagonjwa 124.

Alisema hayo wakati akizungumza kuhusu utendaji wa taasisi hiyo katika mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.

"Wagonjwa wanakuja kutoka nchi za jirani za Afrika Mashariki na Zimbabwe sasa wanafika na Msumbiji," alisema Dk Mwaisalage.

Alisema mashine ya Pet CT-scan ni mradi kubwa wa kimkakati ambao ulianza awamu ya tano, lakini ukamilishaji wake kwa kiasi kikubwa ulifanyika awamu ya sita.

"Ujenzi wa jengo ulianza Juni mwaka jana na utekelezaji utafanyika Machi, mwaka huu na mashine zitasimikwa hadi Juni.”

"Mashine hii ni ya kisasa tutakuwa na mashine mbili ya mionzi dawa kabla hajawekwa kwenye Pet CT-scan na mashine hiyo kwa Afrika Mashariki ipo Kenya tu, lakini hii tunayosimika ni zaidi ya hiyo na Afrika Kusini ipo," alisema Dk Mwaisalage.

Alisema wameweka mfumo wa mashine za kisasa zaidi za 3d na kwamba katika mwaka mmoja wamehudumia wagojwa 326 kuanzia Mei na kuokoa Sh bilioni sita ambazo zingetumika kutibu wagonjwa nchini India ambazo ni takribani Sh milioni 20 kwa mgonjwa mmoja kumaliza tiba.

Dk Mwaisalage alisema Hospitali ya Ocean Road sasa ina chumba cha kuhudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ya mradi wa Covid- 19 na kwamba walipewa Sh bilioni 5.4 kwa ajili ya miradi ya kimkakati.

Alisema mfumo huo ni bora ambao pia umekuwa msaada kwa Hospitali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live