Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ocean Road yakabiliwa na uhaba wa damu

81643 Damupic Ocean Road yakabiliwa na uhaba wa damu

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inakabiliwa na uhaba wa damu hali inayosababisha wakati mwingine huduma kushindwa kutolewa kwa ufanisi.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Ocean Road, Dk. Mark Mseti, amesema kwa siku za hivi karibuni hospitali hiyo imekuwa ikikabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali inayokwamisha utoaji huduma kwa kiwango kinachostahili.

Mseti alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kutokana na tiba zote za mionzi kuhitaji wagonjwa kuwa na damu ya kutosha ili ziweze kufanya kazi sawasawa .

“Tunahitaji chupa za damu 40 hadi 50 kila siku, kuna wakati Mpango wa Taifa wa Damu Salama unaileta kwa kiwango kinachostahili tunapata chupa 50 au 40 na tunaweza kufanya kazi kama inavyostahili lakini hivi karibuni kwa takribani wiki mbili hivi kumetokea upungufu mkubwa wa damu kwenye taasisi yetu. Kwa mfano jana na juzi tulipata chupa zisizozidi 20 kwa siku,” amesema  Dk Mseti.

Katika kujaribu kukabiliana na changamoto hiyo wafanyakazi wa benki ya NMB wametumi mwezi wa huduma kwa Wateja kwa kuchangia uniti 91 za damu.

Dk Msethi amesema kiasi hicho cha damu kitatumika kwa wagonjwa 240 wenye uhitaji wa tiba hiyo.

Pia Soma

Advertisement
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, amesema  lengo la kushiriki zoezi hilo ni kuangalia jinsi ya kuokoa maisha ya watanzania wenzao wenye maradhi hayo.

Amesema  kupitia zoezi walilolifanya linapaswa kuwa wito kwa watanznaia wengine kuona sababu ya kushiriki kuchangia damu.

“Nimetembezwa hospitalini unakuta hata hiyo damu inayohitajika haipo ni kidogo, watanzania tujitolee kuokoa maisha ya wengine,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz