Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ocean Road Hospital imepokea vitanda vitanda viwili vyenye thamani ya Tsh. Milioni 18

21c2655f70b972fb68f751abdfc8bb7a Ocean Road Hospital imepokea vitanda vitanda viwili vyenye thamani ya Tsh. Milioni 18

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imepokea msaada wa vitanda viwili vya umeme nyenye thamani ya Sh Milioni 18 kutoka Jamhuri ya Muungano wa Czech ikiwa ni hatua ya ushirikiano katika kukuza huduma za afya nchini.

Msaada huo umetolewa kupitia kampuni ya Gama Pharmaceutical utawasaidia wahudumu wa afya kuhamisha mgonjwa bila kutumia nguvu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road, Dk.Julius Mwaiselage amesema kuwa taasisi hiyo bado inauhitaji wa vitanda vinavotumia umeme.

“mahitaji ya taasisi ni vitanda 25 vinavyotumi umeme au vya kielektroniki, vilivyokuwepo ni 8 sasa huku bado kuna mahitaji ya vitanda vingine 17 ili kutimia 25.

‘Msaada huuu unamanufaa makubwa sana kwetu katika kutoa huduma hii kwani vitanda hivi vinamsaada mkubwa katika kurahisisha huduma,’ameeleza.

Ameiomba kampuni ya Gama Pharmaceutical iliyoshirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Czech kusaidia kupata vitanda vingine 17 ili kuendelea kutoa huduma inastahili kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Amesema kuwa vitanda hivyo vinahitajika Zaidi katika hospitali hiyo kwani wagonjwa wa Saratani wameongezeka nchini kwa asilimia 60 hadi 70 wanaenda hospitali wakiwa na hali mbaya hadi hawawezi kutembea, hivyo vitanda hivyo vinaweza kufanya kazi nyingi vyenyewe vitakuwa ni mhimu zaidi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Omary Ubuguyu amesema kuwa vitanda hivyo pia vinahitajika katika hospitali zingine kwaajili ya kurahisisha utoaji huduma.

“Sehemu muhimu ni katika hospitali zinazotoa huduma ya dharura, sehemu ambazo zinatolewa huduma za wagonjwa mahututi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz