TAASISI ya saratani ya Ocean Road ya Dar es Salaam imeanza kutoa huduma za urekebishaji mfumo wa nyongo iliyoziba bila upasuaji.
Mfumo huo unapoziba kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo saratani husababisha manjano na muwasho mkali mwili mzima na homa kali wakati mwingine kwa mgonjwa.
Wizara ya Afya kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter, imeeleza kuwa huduma hiyo ilianza kutolewa hivi karibuni na wataalamu wa radiolojia tiba wakiongozwa na daktari bingwa na mbobezi wa radiolojia tiba, Dk Latifa Rajab kutoka taasisi ya saratani Ocean Road.
Huduma hizo hufanywa kwa utaratibu wa mirija kupelekwa kwenye tumbo kwa kuangalia kupitia mashine ya X-Ray na ultrasound ilikuhakikisha imefika na nyongo inaenda katika njia yake.