Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba ndogo, mama wa kambo kunufaika na Bima ya Afya

Nyumba Ndogo Bima Ya Afya.jpeg Nyumba ndogo, mama wa kambo kunufaika na Bima ya Afya

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kufikisha ukaribu wa huduma za afya kwa watanzania hasa watumishi wa umma kwa jamii, Mfuko wa Afya wa Taifa (NHIF) umeboresha huduma zake kwa kuongeza wanufaika wa mbali ili kupata huduma kwa wote kwa kuwaongeza Mama wa Kambo, mke wa pili pamoja na ndugu ama mtoto wa kufikia.

Akizungumza wakati wa kutoa Elimu ya NHIF kwa watumishi Kisarawe Agosti 30, 2022, Dr Lucas Gama alisema kwa sasa huduma za afya zimeboreshwa lengo ikiwa ni kutoa huduma kwa jamii na sio kupata faida Kama ambavyo mifuko mingine ya afya wanavyofanya.

"NHIF ipo kwa Jamii kihuduma sio kifaida kwa hiyo naomba watumishi muifurahie ili kuleta ubora wa mfuko katika huduma sisi bima tunalipia huduma kama miwani ya kusomea.

"Kila baada ya Miaka mitatu kwa kuanzia kwa wanufaika, tunalipia matibabu bora kuliko wengine hivyo naomba watumishi muifurahie huduma zetu na pia tunapokea maoni yenu kwa kufuata utaratibu mzuri uliopo ili kuboresha zaidi," alimazia Dr Gama.

Huu ni utaratibu wa kawaida wa NHIF kuongea na watumishi ili kupokea maboresho na changamoto wanazokutana nazo katika zahanati, hospitali na maduka rasmi ya dawa katika jamii zetu kwa wale wanaotambulika na NHIF.

Mwisho watumishi wa Kisarawe walifurahishwa na ujio wa afisa NHIF kwa lengo la kupeana uzoefu wa huduma za afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live