VIFO vingi vya wanawake wakati wa kujifungua katika Mkoa wa Njombe husababishwa na kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na kifafa cha mimba.
Imeelezwa kuwa hali hiyo inatokana na kuwapo kwa ufinyu wa maarifa na ujuzi duni kutoka kwa wahudumu wa afya kwa kushindwa kutambua mapema dalili za awali za matatizo hayo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kutafakari kuwapo kwa vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa kuwakutanisha wataalamu wa afya wa wilaya zote za Njombe, Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto, Felisia Hyera alisema kuwa licha ya kushuka kwa idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, kutokwa damu na kifafa cha mimba bado ni tatizo kubwa kwa vifo vichache vya sasa.
Hyera alisema Mkoa wa Njombe una idadi ndogo ya vifo vitokanavyo na uzazi ukilinganisha na mikoa mingine nchini.
“Kwa kipindi kati ya Januari na Juni mwaka huu, mkoa wetu umerekodi vifo 23 vya mama na nane kati yao vilitokana na kutokwa na damu na kifafa cha mimba kutokana na shinikizo la damu wakati wa ujauzito,” alisema.
Aliongeza kuwa Wilaya ya Wanging’ombe ilichangia vifo sita vya akinamama.
“Mbali na kuwa na idadi ndogo ya vifo vya akinamama katika mkoa huo, vifo vitokanavyo na uzazi vimeendelea kuwapo ambapo kwa mwaka wa 2019 ilionekana kuwa idadi ya vifo vya uzazi ni 350 ambapo 109 vilitokea wakati wa kujifungua, wakati watoto walifariki dunia kabla ya kuzaliwa 103, waliofariki wakati wa kujifungua ni 112 na vifo vya watoto 26 walifariki baada ya muda tangu kuzaliwa,” alisema.
Katika takwimu hizo, Manispaa ya Njombe inaonesha kuwa na kiwango kikubwa ikifuatiwa na Makambako na wa Wanging’ombe kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo hivyo.
Hyera alisema kuhudhu ria mapema kwa huduma za ujauzito na kujifungua katika vituo vya afya ni kati ya mikakati inayotumika kupunguza vifo vya akinamama kwa sababu kwa njia hiyo watumishi wa afya wataweza kuona dalili za hatari kwa wajawazito na kupata njia bora za kuokoa hali hiyo.
Hyera alishukuru miradi iliyopo mkoani humo ikiwamo Naweza ambayo iko chini ya mradi wa Tulonge Health ambao hutoa elimu ya afya kwa wajawazito na wenzi wao kwenye kutembelea vituo vya huduma mapema ili kupunguza vifo hivyo.
Naye Ofisa Uuguzi wa Mkoa wa Njombe, Sophia Mfungati alisema katika kipindi cha Januari na Juni 2020 mkoa huo ulirekodi idadi ndogo ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi na watoto waliozaliwa ukilinganisha na mwaka wa 2019 kwa sababu ya mahudhurio ya mapema ya kujifungua katika kituo cha afya.
Alisema kwa kuhudhuria na kujifungua katika vituo vya afya wajawazito wanapewa elimu ya jinsi ya kutunza afya zao na za watoto wao na kuongeza kuwa msaada wa wenza wao kushiriki kupiga elimu umechangia kufanikiwa.
Akizungumza katika mkutano huo, Meneja wa Kanda wa mradi wa USAID Tulonge, Elia Ndutila wanayo furaha kuna mradi huo kuisaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa Mkoa wa Njombe.
Mradi huu umefanyika katika kikao 12 ya Tanzania ambapo kupitia majukwaa ya watu wazima ya Naweza kwa lengo la kuhamasisha huduma bora za afya kwa ngazi ya familia na jamii kwa kuondoa mila potofu na kuwapata mbinu za kiafya kujikinga na maradhi kama Ukimwi, malaria, uzazi wa mpango na afya ya uzazi pamoja na ugonjwa wa kifua kikuu.
Mkutano wa kutathimini vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga uliandaliwa na timu ya mkoa ukiwajumuisha waganga wakuu wa wilaya, wataalamu wa afya ya uzazi wa mama na mtoto na viongozi wa mabaraza ya kuboresha huduma mkoani Njombe.