Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimr yashauri Serikali kutenga bajeti kupambana na maradhi yasiyoambukiza

10310 Nmr+pic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Profesa Yunus Mgaya amesema ni vyema Serikali ikatenga bajeti ili kupambana na maradhi yasiyoambukiza.

Akichangia mada katika mjadala wa Mwananchi Jukwaa la Fikra, Juni 28, 2018, Profesa Yunus amesema kuna ongezeko kubwa la maradhi hayo, hivyo jitihada za ziada zinapaswa kufanywa na kila mmoja ili kupambana nayo.

“Lakini bado kuna upungufu, wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu maradhi haya, hizi tafiti zinatakiwa ziwepo wizarani na ziwekwe kwa namna ya kueleweka,” amesema.

Amesema, “Katika tafiti zetu tunazofanya sasa, tunaangalia namna ya kupunguza au kutokomeza kabisa maradhi yasiyoambukiza kwa kuangalia viashiria vinavyosababisha,” amesema Profesa Yunus.

Chanzo: mwananchi.co.tz