Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimr yasema wanawake waongoza kwa unene kupita kiasi

10316 Unene+pic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema asilimia 26 ya wenye umri wa miaka 25 hadi 64 wana unene uliopitiliza, huku idadi ya wanawake ikiwa kubwa zaidi.

Profesa Mgaya ameyasema hayo Juni 28, 2018 wakati wa mjadala wa Jukwaa la Fikra, unaojadili magonjwa yasiyoambukiza ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Alikuwa akijibu swali la mmoja wa washiriki wa Jukwaa la Fikra, aliyetaka kufahamu ni jinsia gani ipo hatarini zaidi kwenye magonjwa yasiyoambukiza.

“Kiwango hicho cha wenye unene kupita kiasi kina uhusiano wa karibu na shinikizo la damu,” amesema.

Kuhusu suala la kuandika ripoti zao katika lugha rahisi, mkurugenzi huyo amesema tayari NIMR inafanya hivyo katika tafiti zao na wataendelea kufanya hivyo ili wananchi wa kawaida waelewe maudhui yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz