Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni mazoezi kabla au baada ya kifungua kinywa?

Ni mazoezi kabla au baada ya kifungua kinywa?

Thu, 5 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Je, unapaswa kufanya mazoezi asubuhi kabla ya kifungua kinywa  au baada?

Hayo ni majadilino ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka kadhaa sasa miongoni mwa watu wanaopenda kufanya mazoezi ili kuijenga miili yao na kuwa na afya bora.

 Kula kabla ya mazoezi inaelezwa kupandisha sukari na kuupa mwili mafuta, lakini hata hivyo unaondoa uchovu na kizunguzungu.

Lakini kula baada ya mazoezi unachoma mafuta zaidi. Utafiti mdogo uliochapishwa hivi karibuni Uingereza  umeeleza kuwa watu waliofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa walichoma mafuta mara mbili zaidi kuliko wale waliofungua kinywa na kufanya mazoezi.

“Kundi linalofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa linakuza uwezo wa insulin kufanya kazi, lakini makundi yote yatapoteza kiwango sawa cha uzito,” anasema mtaalamu wa mazoezi  Javier Gonzalez kutoka kitengo cha afya cha Chuo Kikuu cha Bath.

Hata hivyo, daktari wa binadamu Samwel Shita katika safu yake ya mazoezi aliwahi kusema kuwa mtu anapofanya mazoezi huupa mwili nafasi ya kutoa taka sumu kupitia jasho.

Chanzo: mwananchi.co.tz