Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngariba Simanjiro wajisalimisha, wakabidhi visu

Ngariba Baadhi ya mangariba waliojisalimisha hivi karibuni wakiwa na Dk.Gwajima

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Caroline Mtapula amewataka mangariba katika Wilaya ya Simanjiro kuacha kukeketa watoto wa kike na kuwaozesha wakiwa katika umri mdogo kwani wanahaki ya kupata elimu, ni haki ya kila mtoto kike kupata elimu.

Mtapula amesema kuwa mtoto wa kike anayestahili kwenda shule asiache kupelekwa shule kupata elimu na kumpeleka kwenda kuolewa tutakuwa tunamnyima haki yake na tutakuwa tunajinyima haki akinamama.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt. Suleimani Serera amewaasa wananwake katika wilaya hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais Samia katika kuisimamia Serikali, ambapo amewataka kuvunja mfumo unaowakandamiza wanawake katika jamii. Nao mangariba 37 katika Wilaya ya Simanjiro wamejisalimisha na kukabidhi visu ambavyo wamekuwa wakitumia kukeketa watoto wadogo hasa jamii ya kimaasai kutokana na kile walichodai ni matokeo ya elimu na maendeleo katika jamii.

Mwenyekiti wa Ngariba hao, Naserian Alais amekabidhi kisu kwa niaba kwa Katibu Tawala Mtapula, akitaka jamii na wakunga wanaojishughulisha na ukeketaji kuacha kazi hiyo ambayo inaathiri haki na utu wa mtoto wa kike.

Kilichotufanya tukabidhi kwanza tulipata elimu na tukaona ya kwamba tunawanyayasa watoto wakike kabla hawajajitegemea au hawajapata uwezo wa kujua kuwa ukeketaji niunyanyasaji kwa watoto wa kike, ambapo amtoa wito kwa jamii ya wamasai kuacha ukeketaji kwa watoto wa kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live