Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugulile aupa siku saba uongozi Mawenzi Hospitali

28380 Mawenzi+pic TanzaniaWeb

Fri, 23 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na kubaini mashine muhimu za vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo ya kupima kiwango cha CD4 kutofanya kazi kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Hayo yamebainika leo Alhamisi Novemba 22, 2018 baada ya naibu waziri huyo kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kukagua idara mbalimbali, wodi za wagonjwa na miradi inayotekelezwa na Serikali katika hospitali hiyo.

"Inakuaje uongozi wa hospitali mnakaa kimya wakati mashine za CD4 hazifanyi kazi. Inasikitisha sana maana hospitali hii ni kubwa na inategemewa na wananchi wa mkoa huu,” amesema.

Kufuatia hali hiyo Ndugulile ametoa wiki moja kwa uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha mashine hizo zinafanya kazi na huduma zinarejea mara moja kwa wagonjwa.

"Nimekuja hapa nimekuta mafundi wanafanyia kazi mashine hizi mbovu. Naomba mhakikishe zoezi hili linafanyika haraka ili huduma zitolewe mapema kwa wagonjwa,” amesema Ndugulile.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Japhet Boniface ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na naibu waziri huyo na kuhakikisha huduma zinarejea mara moja.

Dk Boniface amesema hospitali hiyo inakabiliwa na ukosefu wa madaktari bingwa wa magonjwa ya akili.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz