Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namna ya kudhibiti uchovu viungo

9459 Shita+Samweli TZWeb

Mon, 18 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika maisha ya kila siku ni kawaida kwa mfanyaji wa mazoezi au kazi ngumu kuwahi kupata hisia za uchovu wa viungo vya mwili kiasi cha kujihisi kuwa ana ugonjwa mkali.

Uchovu hujulikana kitabibu kama Muscle fatigue au Physical fatigue ni hali inayojitokeza mwilini pale misuli ya mwili inapofanyishwa kazi kupita kiwango chake.

Kujitokeza kwa uchovu unao ambatana na maumivu ni njia mojawapo ya mwili kujihami na kukupa ishara kuwa viungo vya mwili ikiwamo misuli imetumika kupita kiasi.

Uchovu unasababisha misuli ya mwili kukosa nguvu kama ilivyo kawaida yake. Tatizo hili linaweza kuambatana na maumivu yanayoweza kuwa ya wastani mpaka kuwa makali.

Hisia za uchovu huweza kuhisiwa zaidi katika maeneo ya maungio (joint), mgongoni, kiunoni, mapajani na magotini.

Muathirika anaweza kuhisi pengine ana ugonjwa mkubwa kumbe tu ni uchovu wa viungo vya mwili.

Uchovu unatokana na uwapo vitu vinavyoingilia hatua za utendani yaani kukunjuka na kujikunja kuwezesha matendo mbalimbali ikiwamo kukimbia, kuruka na kutembea.

Tatizo hili linaweza kusababishwa na mishipa ya fahamu kutosisimua vizuri misuli na uwepo wa mrundikano wa mabaki au taka mwili baada ya seli kutumia sukari ya mwili kupita kiwango chake.

Uchovu unaotokana na mwili kufanya kazi sana ni tatizo la muda tu ambalo linaweza kuisha endapo mambo mbali mbali yatafanyika.

Unapokuwa na uchovu unahitajika kulala masaa 6-8 pasipo usumbufu wowote ili kuepuka kukatika katika kwa usingizi.

Pumzisha mwili katika maeneo yenye hewa safi ikiwamo ufukweni au maeneo ya wazi kwani mazingira ya hewa chafu yanachangia kuongeza uchovu zaidi.

Kula mlo kamili ikiwamo vyakula vyenye protini, mboga za majani na matunda na vyakula vya wanga.

Lishe hii inasaidia kukurudishia nguvu iliyotumika, kurudishia akiba ya nishati katika misuli na kuwezesha ukarabati na uponaji wa vijeraha vya misuli.

Kunywa lita 1.5-3 kabla ya kufanya mazoezi magumu na fanya mazoezi mepesi kwa dakika 5-10 kabla ya kuanza mazoezi au shughuli za kila siku.

Fanya mazoezi ya viungo ya kunyoosha misuli ya mwili angalau dakika 10-15 huku ukiwa katika mkao sahihi kimwili ili kuondoa uwezekano wa kujijeruhi misuli.

Fanya huduma ya usingaji au utomasaji (massage) kwa mafuta ya kuchua ili kulainisha misuli na kuwezesha damu kutirika kwa wingi katika misuli ili kuzidondoa taka mwili au mabaki kirahisi katika misuli.

Oga kwa maji ya vuguvugu yanayotiririka kwa wingi au oga katika mabafu ya kisasa yenye kutoa mvuke wa joto.

Epuka mambo yatakayokupa shinikizo la akili au kukusababishia hisia hasi kwani yatakuongezea uchovu. Jichanganya katika mazingira ya burudani ili kukupa hisia chanya.

Chanzo: mwananchi.co.tz