Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri Ndugulile aikagua NIMR

61731 NMRI+PIC

Sun, 9 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), kuboresha ukusanyaji wa takwimu katika tafiti za magonjwa ya binadamu zinazofanyika ikiwemo magonjwa ya dengue na kipindupindu.

Amesema kuboresha ukusanyaji huo takwimu utasaidia kutambua idadi halisi ya wagonjwa pamoja na vifo vinavyotokea katika jamii hali itayosaidia kuboresha utoaji huduma nchini.

Dk Ndugulile ameyasema hayo Leo Ijumaa Juni 7, 2019 alipofanya ziara ya kukagua hali ya utendaji kazi katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mbali na hayo, Dk Ndugulile ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika nyanja zote Hususan katika utoaji taarifa za utendaji kazi kwa jamii na uongozi wa namna taasisi hiyo inasaidia kutatua matatizo katika jamii.

Aidha, amesema ni muhimu kwa taasisi hiyo kushirikisha viongozi wa kisera katika shughuli zao ili kutambua mafanikio na changamoto za taasisi hiyo jambo litakalorahisisha kutatua changamoto zinazoikumba taasisi hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya amemshukuru Dk Ndugulile kwa kufanya ziara katika Taasisi hiyo na ameahidi kutekeleza maagizo yote ndani ya muda mfupi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz