Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri Afya amfyeka daktari Siha

Tz Data Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameonyesha kukasirishwa na huduma mbovu inayotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha baada ya wananchi kulalamikia huduma mbovu huku akikiri kujionea kwa macho yake baada ya kushuhudia mgonjwa akiachwa zaidi ya saa moja bila kuhudumiwa.

"Ninaagiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha aondolewe katika nafasi hiyo abaki kama Daktari wengine, nilifika hapa zaidi ya mara sita na jana nimekuja tena nikakuta Askari aliyepata ajali akiwa ametelekezwa bila msaada wowote," - Dkt MolIel.

Imekua ikiripotiwa sehemu mbalimbali nchini wananchi wakilalamikia uduni wa lugha na huduma toka kwa wahudumu wa afya hivyo kupelekea maamuzi ya viongozi kuwashushia rungu na wengine kuhamishwa vituo vya kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live