Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Spika awashangaa wanaume wanaoenda kupima DNA ‘kitanda hakizai haramu’ (+video)

Video Archive
Fri, 6 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amewakumbusha wanaume kwa kuwatania kuwa hakuna umuhimu wowote kwa wao kufuatilia kipimo cha DNA ili kuweza kuthibitisha mtoto ambaye anamlea ni wake au laa kwa kuwa kitanda hakizai haramu.



Mhe. Tulia ametoa kauli hiyo ya kuwafikisha ujumbe kwa baadhi ya familia wanaokumbwa au kusumbuliwa na kadhia hiyo katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha tatu kinachoendelea mkoani  Dodoma wakati alipokuwa anafunga kipindi cha maswali na majibu  leo Aprili 5, 2018.

“Nilidhani wanawake tunataka kuandamana humu ndani Bungeni, watu tuna watoto wengi humu lakini kiswahili cha kawaida kabisa kinasema ‘kitanda hakizai haramu’ sasa unaenda kumpima wa nini”, amesema Ackson.

Hatua ya Dkt. Tulia kutoa kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kuhoji kuwa, “Kwakuwa takwimu zinaonyesha zinaonyesha kwamba kila watoto wanaozaliwa watoto wanne sio wa baba muhusika, Je? Serikali inaonaje juu ya udhalilishaji wa kina baba kwakubambikiziwa watoto ambao sio wa kwao kigenetic.

Chanzo: bongo5.com