Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yasaidia ujenzi kituo afya cha corona

NMB Pic Ed.webp NMB yasaidia ujenzi kituo afya cha corona

Fri, 5 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Makambini Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kusaidia kukabiliana na janga la ugonjwa wa corona.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Meneja wa NMB Tawi la Mbalizi Road, Hamadan Silliah, amesema msaada wa vifaa hivyo ni moja kati ya mpango wa NMB ya kutenga sehemu ya faida yake katika kusaidia huduma za kijamii.

Alisema walipokea maombi ya kusaidia ujenzi wa kituo hicho, na kwamba moja kati ya sera za benki ni kurejesha faida katika huduma za kijamii ni pamoja na kusaidia katika kukabiliana na majanga na huduma za afya.

Alisema kutanuka kwa huduma za benki hiyo kumeongeza pia uwapo wa huduma za NMB mkononi kupitia simu za kiganjani na hii imesaidia kufanya muamala kwa njia za kidijitali ikiwa ni moja ya sehemu ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Regina Bieda, alisema ujenzi wa kituo hicho kinachotarajiwa kuwa na wodi mbili za kinamama na wanaume kinatarajia kugharimu kiasi cha Sh. milioni 95.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Said Irando, alisema kuwa benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika huduma za kijamii na kuwa msaada katika kituo hicho cha afya ni mahsusi kwa magonjwa ya milipuko.

Alisema kituo hicho kipo mpakani ambayo ni njia kuu kuelekea nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), hivyo kumekuwa na mwingiliano wa wageni kutoka nchi zilizopo kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kuwa awali kituo hicho kilitengwa kwa ajili ya ebola na sasa kinaboreshwa kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live