Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NIMR yatakiwa kufanya utafiti zaidi magonjwa ya mlipuko

7a5975933a9bec235ac6767c6b71c897.jpeg NIMR yatakiwa kufanya utafiti zaidi magonjwa ya mlipuko

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafi ti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuendelea kufanya tafi ti za magonjwa ya milipuko yanapojitokeza kudhibiti athari zake kwa jamii.

SERIKALI imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafi ti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuendelea kufanya tafi ti za magonjwa ya milipuko yanapojitokeza kudhibiti athari zake kwa jamii. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alitoa mwito huo wakati maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo zilizofanyika jana jijini Tanga. Aliitaka taasisi hiyo kufanya jitihada za kutafiti magonjwa yanapojitokeza sehemu nyingine katika dunia kabla ya kufika nchini. “NIMR niwapongeze mlifanya kazi kubwa wakati wa corona …Endelea na juhudi hizo kwani mmebeba mustakabali wa taifa hili,” alisema Shigela. Aidha alisema kuwa wakati huu ambao taasisi hiyo inatimiza miaka 40 kwa kiasi kikubwa wameweza kutoa mchango mkubwa katika sekta ya afya. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk Mercy Chiduo alitaja mafanikio makubwa yaliyoweza kufikiwa kutokana na utafiti za ugonjwa wa malaria hadi kusaidia kubadilishwa kwa tiba kutoka kwenye dawa moja hadi mseto. “Kutokana na tafiti katika ugonjwa wa malaria tumeweza kupunguza vifo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 ikiwemo kudhibiti maambukizi na kuboresha kinga zao dhidi ya ugonjwa huo,”alisema Chiduo. Aidha, aliiomba Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii Jinsia, Wazee na Watoto kutenga bajeti kwa ajili ya taasisi hiyo ijitegemee katika kufanya tafiti zake badala ya kutegemea wahisani. Daktari mstaafu katika kituo hicho, Dk Acleus Rutta alisema licha ya NIMR kufanya kazi kubwa ya kudhibiti na kuratibu tafiti zote hapa nchini zenye tija ipo haja kwa serikali kuanza uwekezaji kwenye tafiti.

Chanzo: habarileo.co.tz