Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NIMR wapewa siku 14 kutoa ripoti ya Kansa Kanda ya Ziwa

NIMR wapewa siku 14 kutoa ripoti ya Kansa Kanda ya Ziwa

Wed, 6 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Serikali imeipa wiki mbili kwa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kukamilisha na kutoa taarifa ya utafiti kwanini mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa idadi ya wagonjwa wa saratani nchini.

Agizo hilo limetolewa jijini Mwanza leo Jumatatu Novemba 4, 2019 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alipozungumza na Waganga Wakuu wa mikoa, Wilaya, Watafiti wa wa magonjwa ya binadamu na wadau wa sekta ya afya kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Wakati wa wa ziara yake mkoani Mwanza Julai 15, 2019, Rais John Magufuli alizungumzia tatizo la ugonjwa wa kansa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa; kwetu sisi wasaidizi na watendaji hilo lilikuwa ni amri ya kutafuta kiini na ufumbuzi wa suala hilo na najua tunaifanyia kazi, Sasa tuikamilishe ndani ya wiki mbili zijazo ili ripoti itoke,” amesema na kuagiza Dk Ndugulile

Amesema taarifa ya utafiti huo siyo tu utaonyesha uwepo wa tatizo kama lipo, bali pia kutasaidia kufahamu kiini na nini kifanyike kukabiliana na nalo.

Akizungumza baada ya kuzindua miradi saba ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza Julai 15, 2019, Rais Magufuli aliagiza taasisi na mamlaka husika kufanya utafiti kuhusu taarifa za tatizo la ugonjwa wa kansa kuongezeka katika mikao ya Kanda ya Ziwa.

Katika hotuba hiyo iliyorushwa moja kwa moja na Kituo cha Taifa cha Luninga (TBC), Rais Magufuli alisema mikoa hiyo ya Mwanza, Kagera, Shinyanga Mara, Simiyu na Geita inaaminika kutoa asilimia 50 ya wagonjwa wote wanaotibiwa katika Taasisi ya Taifa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Wakati Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Tafiti kutoka NIMR, Dk Paul Kazyoba akielezea matumaini ya tafiti za afya kutoa kusaidia mabadiliko chanya katika sekta ya afya, Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dk Thomos Rutachunzimbwa ameahidi kuwa agizo la Naibu Waziri litafanyiwa kazi ndani ya muda ulioagizwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz