Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NIMR mbioni kuzalisha vidonge vya mitishamba

Eb24064abdb121af7e21685e9ec5bcdb.jpeg NIMR mbioni kuzalisha vidonge vya mitishamba

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Taifa ya Utafi ti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imewezeshwa na serikali kusimika mitambo itakayoisadia kuchakata mazao ya miti ambayo ni dawa kwa ajili ya kuzalisha vidonge, dawa za unga na dawa za maji kwa ajili ya tiba ya magonjwa mbalimbali.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya NIMR, Profesa Yunus Mgaya wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Ardhio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu miaka 40 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

Alishukuru serikali kwa kuiwezesha taasisi hiyo kuzalisha dawa za tiba asili na tiba mbadala na kutumia rasilimali za miti kwa kuiwezeshwa kifedha kusimika mitambo itakayosaidia kuchakata mazao hayo ya miti ambayo ni dawa kuzalisha vidonge, cdawa za unga na dawa za maji.

Alisema dawa zitakazolishwa kupitia mtambo huo zitazalishwa katika mazingira salama, ya usafi na zitafanyiwa utafiti kuhakikisha kujihakikishia kuwa zina usalama na ufanisi wa kutibu.

“Sasa tutaweza kunywa kidonge kimoja au viwili au kijiko kimoja, tutafikia uwezo wa kutoa matibabu ambayo yanalenga vipimo halisi kwa ugonjwa ambao mtu anaumwa na kumpa dawa katika mazingira salama,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema katika kufanikisha suala hilo la tiba asili na tiba mbadala, taasisi hiyo itashirikiana kwa karibu na watalaamu wa tiba asilia Tanzania ambao wana maarifa makubwa ya tiba asilia na tiba mbadala.

Alisema NIMR tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya tafiti ya dawa za asili kwa sababu sheria inaipa taasisi hiyo majukumu kufanya utafiti wa tiba mbadala na tiba asili ili kuleta tija katika kupunguza magonjwa na kutibu watu.

“Lengo kubwa la kipengele cha sheria ni kuwezesha taifa kutumia rasilimali zake ikiwemo miti na mimea. Dawa karibia zote zimeanzia kwenye mimea baadaye ikionekana inafaa ndio inahama na kutengenezewa kimaabara na Tanzania tuna utajiri mkubwa wa mimea,” alisema.

Akielezea taasisi hiyo ilivyoshughulikia ugonjwa wa corona, Profesa Mgaya alisema iliamua kushirikiana na wananchi na serikali katika mapambano dhidi ya corona kwa kutumia njia mbadala za kufukiza na kutengeneza tiba lishe NIMR CAF iliyoleta matokeo chanya kwa watumiaji.

“Mpaka sasa hakuna dawa ila sasa hivi ndio kuna majaribio ya chanjo na nyingine zinaanza kuingizwa kwenye soko…Wananchi waliitumia NIMR CAF wakapata matokeo chanya na kujenga imani na uwezo wa tiba asili katika kupambana na magonjwa,” alisisitiza.

Katika kipindi cha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mkurugenzi huyo alieleza kuwa taasisi inajivunia tafiti mbalimbali za tiba na kinga iliyofanya na kupata mafanikio.

Alitaja baadhi ni pamoja na utafiti uliofanywa na kituo cha NIMR cha Amani Tanga mwaka 1990 wa kuangalia uwezekano wa kutumia viuatilifu kwenye vyandarua na ikathibitika kuwa vyandarua vikiwekwa dawa kiwandani vina uwezo wa kumkinga mtu sipate maambukizi ya malaria.

“Pia katika eneo hilo la malaria talifanya utafiti wa mabadiliko ya dawa ya klorokwini iliyookuwa tayari inaonesha usugu na kwenda kwenye dawa ya mseto,” alisema.

Mpango huo wa kuzalisha dawa kutokana na kuchakata miti, ni unadhihirisha serikali ya awamu ya tano ilivyodhamiria kuboresha sekta ya mitishamba kama ambavyo Rais John Magufuli amekuwa akihimiza juu ya hilo.

Wakati wa uzinduzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma, Magufuli alisema serikali yake inakusudia kuimarisha kitengo cha utafiti wa tiba mbadala na kuruhusu matibabu na maduka rasmi ya dawa za asili nchini hatua iliyokonga mioyo ya wadau wa tiba mbadala na tiba asili.

Chanzo: habarileo.co.tz