Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHIF yatoa semina elekezi kwa vyama vya wafanyakazi

2607aa0b7ffe95786ef6e4e5090db1ee NHIF yatoa semina elekezi kwa vyama vya wafanyakazi

Sat, 20 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Mwanza umetoa semina ya siku mmoja kwa vyama vya kazi mkoani hapa kwa lengo la kujengeana uwezo kuhusiana na shughuli mbali mbali zinazofanywa na mfuko katika kugharamikia matibabu ya Wanachama wake.

Akizungumza wakati wa Semina hiyo, Meneja wa mfuko huo mkoani hapa Jarleth Mshashu alisema mfuko wao utaendelea kutoa elimu ya mfuko wa Bima ya Afya na mabadiliko ya sera.

Aliahidi wataendelea kutekeleza sheria mbali mbali za mfuko huo. Mshashu alisema kumekuwa na changamoto baadhi ya watoa huduma wanaleta madai ya udanganyifu lakini mfuko wanao utaratibu wa kuzuia wizi.

Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza,John Magazeti alisema wafanyakazi wanatakiwa kujiunga na mfuko wa Afya(NHIF) ili kupunguza gharama za matibabu kutokana.

Amewaomba watumishi wa nhif kuhakikisha wanafika katika ofisi mbali mbali kwajili ya utoaji Elimu za mfuko wa bima ya huduma za Afya.

Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilayani Ilemela Benjamin Bulugu alisema kumekuwa na changamoto ya uongezekaji wa gharama ya dawa kutoka kwa watoa huduma. Ameiomba nhif wawe wanasaidia kulipia gharama za mazishi pale mwanachama wake anapofariki.

Ofisa udhibiti ubora wa nhif,Dk Julieth Muhanika alisema Bado kumekuwa na uelewa mdogo sana kuhusu dhama ya mfuko wa bima ya Afya(NHIF).

Alisema pia kumekuwa na tatizo la mfumuko wa bei ya dawa kutoka watoaji huduma. Alisema bei za dawa hazitabiriki zimekuwa zinapanda mara kwa mara.

Chanzo: habarileo.co.tz