Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHIF yatangaza maboresho huduma ya bima

Nhif NHIF yatangaza maboresho huduma ya bima

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo Februari 28, 2024 umetangaza maboresho ya kitita kipya na bei za huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza dawa mpya 247 ambazo hazikuwepo tangu kitita hicho kupitishwa mwaka 2016, kwa Lengo la kufikia mahitaji ya wanachama kwa kuzingatia hali halisi ya maendeleo ya sekta ya afya nchini na kwa kuzingatia tafiti za kisayansi zilizofanyika.

Mkurugenzi wa NHIF, Dkt. Bernard Konga amebainisha hilo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea miaka 24 ya utoaji huduma wa mfuko huo, ambapo kitita hicho kilichogusa maeneo matatu muhimu, kitaanza kutumika kuanzia Machi 1, 2024.

Amesema Kitita hicho kitakuwa na manufaa kwa Wanachama wanaotumia dawa za 'Pressure' na sukari sasa kuweza kupata dawa katika ngazi za chini, Wanachama wanaopata 'dialysis' gharama imeshushwa chini, Huduma za kibingwa na bingwa bobezi kama matibabu ya moyo, saratani, figo kupatikana kwenye ngazi za Kanda na kuondoa changamoto ya kukosa dawa vikituoni.

Maeneo yaliyoguswa na kitita hicho kipya ni pamoja na huduma ya usajili, ushauri na wakati wa kumwona daktari, pili huduma ya dawa na eneo la tatu na mwisho ni huduma za upasuaji na vipimo.

“Hatujabadilisha gharama ama ada ya mwanachama kujiunga na mfuko wa NHIF. Tulichoboresha ni malipo ya NHIF kwa watoa huduma kwa niaba ya mwanachama,” amesema Dkt. Konga na kuongeza.

“Tutapita kutoa elimu kanisani, mskitini mashuleni na maeneo mengine. Kwakuwa Serikali imeamua kumkomboa mwananchi ni lazima kuwe na Bima ya afya kwa wote.” Amesema kiongozi huyo.

Kuhusu Kipeperushi kilichotolewa na watoa huduma za Afya Juu ya mpango wa Maboresho ya kitita cha Huduma za Bima, Mkurugenzi mkuu huyo wa NHIF amesema Serikali bado haijafunga milango ya Kupokea maoni au Ushauri kuhusu Maboresho hayo ya Kitita cha Huduma za Bima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live