Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHIF yajipanga kuongeza wanachama wapya

1125b4b2b30326c59059e897ad244730 NHIF yajipanga kuongeza wanachama wapya

Thu, 24 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga amesema mfuko wao upo katika mpango wa kuhakikisha unaongeza wananchama wapya.

Konga alisema hayo wakati wa mkutano wa siku moja na watoa huduma katika mkoa wa Mwanza. Alisema Jukumu lao ni kuhakikisha wanaendelea kuwatafuta na kuwandikisha wanachama wapya.

Alisema pia watajipanga kuhakikisha wanalipa madai ya wanachama wao.

‘’Tumepata malalamiko kuwa tunachelewa kulipa madai kama mfuko tumeanzisha utaratibu kuwa kila kituo kina uwezo wa mwanachama wetu kuwakilisha madai yake siku hiyo hiyo’’ Konga alisema.

Alisema Mfuko wao utaanza kuyafanyia kazi na kuona madai ya wanachama wao ni stahiki na kulipa madai yote ndani ya siku 14 kwa kuwa mfuko wao una uwezo wa kulipa.

Alisema wamekuwa wakipokea madai mengi kutoka kwa watoa huduma wao lakini madai hayo yamekuwa na viashiria vya wizi au ubadhilifu kwa sababu watoa huduma wamekuwa wanadai tofauti na fedha walizotoa.

Kwa upande meneja wa NHIF Mwanza,Jarlath Mushashu alisema wataendelea kulipa madai ya watoa huduma na kutengenza kadi za wanachama.

Alisema mkoa wa Mwanza una zaidi ya vituo vya kutolea huduma 590 lakini vilivyosajiliwa na kutambulika ni vituo 390.

‘’Tumesajili vituo vipya 12 na zaidi ya vituo 100 vimeweza kuboresha mikataba yao. Katika mwaka 2019/2020 tumelipa zaidi ya bilioni 12.6 kwa watoa huduma wetu kama ofisi ya mkoa wa Mwanza’’ alisema Mushashu.

Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk Elias Misana alisema mkutano huo na watoaji huduma utasaidia sana katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili watoa huduma

Chanzo: habarileo.co.tz