Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHIF yajibu tuhuma dhidi yake

Ef1f33245021fe4ce7890a6e07c42a0a NHIF yajibu tuhuma dhidi yake

Thu, 3 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu amekanusha tuhuma za shirika lao kuendesha utaratibu feki wa makato ya fedha kwa hospitali na zahanati binafsi mkoa wa Mwanza na kusababisha hasara na kilio kikubwa kwa wamiliki wa hospitali hizo.

Tuhuma hizo zilizoripotiwa zinamuhusisha msimamizi wa fedha wa shirika hilo mkoani Mwanza Julieth Muhanika na meneja wa NHIF mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu. Mushashu alisema hawahusiki na madai hayo bali si ya kweli kutokana na shirika lao hufanya kazi kwa utaratibu na kanuni.

Alisema shirika lao halijawahi kushawishi watoa huduma au wamiliki wa kituo chochote cha Afya kutoa wala kupokea rushwa. Alisema anawaomba watoa huduma wote kupeleka orodha yao ambao wanaihisi kuwa walikatwa malipo yao yasiokuwa halali na haki iweze kupatikana.

Akijibu kuhusu kunyanyasa wateja wao katika kipindi cha miaka miwili cha 2019 na 2020 Mushashu alisema hajawahi kufanya unyanyasaji wa aina yoyote kwa watoa huduma wa katika mkoa wowte akiwa Mwanza,Moshi au mkoa wa Simiyu.

Alisema watoa huduma na wamiliki wa vituo vya Afya wawe wanaomba taarifa juu ya makato yao kupitia ofisi yao. Mushashu alisema kama mtoa huduma atakuwa hajaridhika kuhusu utoaji huduma wao ni bora waandike kwenye sanduku la maoni.

Chanzo: habarileo.co.tz