Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewataka wanachama wake kutokubali kulipishwa zaidi “topup” katika gharama za matibabu kwenye vituo vya afya baada ya Mfuko huo kuanza kutekeleza kitita kipya kilicho boreshwa cha huduma za afya.
Mkurugenzi wa Tiba na Huduma za Kitaalam wa NHIF, Dk. David Mwenesano amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa bei mpya zilizopitishwa na Mfuko huo zimezingatia kikokotoo cha kisayansi kilichoangalia gharama za uzalishaji na uendeshaji.
“Bei hizi hazihitaji topup. Tumekuja na bei hizi kitaalamu kwa kuangalia uhitaji wa kila utaratibu (procedure) na wataalamu wa hizo huduma,” amesema Dk Mwenesano na kuongeza: “Hatuhitaji ya aina yoyote kwa mwanachama.”