Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBTS wazindua kampeni ya kitaifa ya "Uchangiaji Damu"

Damu Pc Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu kutoka Mpango wa Taifawa Damu Salama Dk. Avelina Mgasa.

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Mpango wa Taifa wa Damu Salama nchini (NBTS) umezindua kampeni ya kitaifa ya kuihamasisha jamii kuchangia damu, huku ukilenga kukusanya chupa 19,514 kutoka kwenye timu zao 226 zilizopo nchi nzima.

NBTS imefikia hatua hiyo ili kuokoa vifo vya wajawazito vinavyotokana na kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Takwimu za vifo vya uzazi za Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee zilizokusanywa kati ya Januari hadi Desemba mwaka 2020 zinaonyesha asilimia 26.3 ya vifo vingi vya wajawazito vilisababishwa na kutoka damu nyingi baada ya kujifungua.

Akizungumzia kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2021 Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika mpango huo, Dk. Avelina Mgasa amesema kampeni hiyo imeanza Jumatatu Septemba 20, 2021 katika kanda zote saba za kukusanya damu nchini.

Amesema kampeni hiyo inailenga jamii kuwa wachangiaji wa damu, kwani asilimia 80 ya damu inayokusanywa nchini inatoka kwa wanafunzi na vijana wanapokuwa shule na vyuoni.

Dk Mgasa amesema kaulimbiu ya kampeni ya mwaka huu ni ‘Changia damu kuokoa wanaoleta uhai duniani’ ina lengo la kuhamasisha jamii kutoa damu kwa hiari, ili kuokoa maisha ya wajawazito.

“Kampeni hii inalenga kuongeza upatikanaji wa damu salama ambayo itasaidia kuokoa maisha ya kinamama ambao hupoteza maisha kila siku kutokana na matatizo ya uzazi na wakati wa kujifungua,” amesema.

Chanzo: Mwananchi